Wanachama wa THISDASO wanaendesha efoti kubwa katika kijiji cha Ngarenanyuki. Mkutano huo unahudumiwa na Ndugu Jerard Nyaonge (mahubiri) Juma Kibona (Kaya na familia pamoja na Usiku Projecta) na Mchungaji Mahemebea (Afya) ilianza February 5/2012 na unatarajiwa kuisha tarehe 18/2/2012.
Mbinu kadhaa zimeibuliwa kama njia ya kufanikisha mkutano huo ni pamoja na kushiriki kuvuna mashamba ya nyanya na mahidni kwa wanakijiji wa Kijiji cha Ngarenanyuki.
Njia nyingine ni kufundisha katika shule ya sekondari ya Momela ambapo walimu bila kujijua wamejikuta wakiwaachia vipindi vyote wana THISDASO ambao wamepanga ratiba upya na kutawala shule yote huku wakimchagua Headmaster wa muda (Salim Nyisarya).
Moja ya mkakati ni kuwataka wanafunzi wote kuhudhuria vipindi vya efoti kama sehemu ya masomo yao. Kwa mkakati huo baadhi ya wanafunzi wamejikuta wakiomba kubatizwa.
kusaidia wenye shida, kujitolea kufundisha, kuvuna mashamba ya wanakijiji hizi ni mbinu ambazo zimefaulu sana.
habari hizi zinapatikana pia thisdasouniversiotyofarusha.blogspot.com
wawakilishi wa chama cha THISDASO wakiwa wametoka kumpa babu na bibi zawadi za nguo na vyakula tele tele kutokana na michango ya wanachama. |