Thursday, February 2, 2012

NAWASALIMU KATIKA JINA LA BWANA.
                  Taarifa za hivi karibuni zinasema kuwa asubuhi ya Ijumaa ya tarehe 3/2/2012 vijana wa THISDASO wameondoka kwenda Ngarenanyuki kwenye efoti wakati wengine wakiwa wanaelekea Makwao. Akihojiwa mmoja wa wanachama hao aitwaye Leah Karangi amesema "ni kutokana na kuendea mahitaji kwa wazazi inatulazimu kwenda makwetu" Hata hivyo mjumbe wa programu zote Aunt Masegenya au Mama Mkingira naye alikaririwa akisema "Ninawatakia wanachama wote effort njema" Huku akionesha kutamani kuhudhuria.
                              Vijana wa Kisabato wapatao 85 wanahudhuria mkutano huo, aidha mafundisho ya Neno la Mungu yataongozwa na Mwalimu Nnyaonge, Semina za Afya zitaongozwa na Mchungaji na Mwasitete na Semina za Kaya na Familia zitaongozwa na Mwalimu Kibona kutoka Mpanda. Unatarajiwa kuwa mkutano wenye mafanikio.

No comments:

Post a Comment