Monday, February 6, 2012

MKUTANO WAPAMBA MOTO


WATU 86 WAUNGUA KWA MOTO NGARENANYUKI NA 7 KUFA.

Na Juma Kibona – Mawasiliano THISDASO UOA.
Katika mkutano wa efoti uliofanyika jana 6/2/2012 hapa Ngarenanyuki-USA River – Arusha, watu 86 (watu wazima wageni tu) walihudhuria na hakika walichomwa na neno la Mungu linaloweza kuchoma kila moyo wa mwanadamu. Ilipofika mwisho wa mkutano watu 7 waliamua kuifia dhambi na kufufuka katika utukufu wa Bwana. Aidha wanakijiji hawa, wamekiri kuwa Yesu anawapenda sana. Frolida anasema, “Nimekuwa nikisumbuka sana ili nipate mme nimekuja kuombewa ili niolewe”. Watu wa Mungu waliomba naye na akafurahi kwamba bila shaka Bwana atafanya muujiza.
Efoti hii inaendesha na kusimamiwa na wanachama wa THISDASO tawi la University of Arusha. Mkutano huu ulianza tarehe 5/2/2012 na utamalizikia tarehe 18/2/2012. Mkutano huu umeambatana na matembezi. Ambapo kila siku asubuhi wanachama hawa hutembelea wanakijiji wote wa Ngarenanyuki.
Leo 7/2/2012, kati ya waliotembelewa na Mzee “Selewani” Silvano ambaye ana miaka 130 kama alivyosema. Mzee huyu anasema, “Nilikuwa na watoto 6, wanne kati yao walikuwa wa kiume na walikwishafariki wote kwa tatizo la UKIMWI, wamebaki 2 wa kike ambapo mmoja hajulikani alipo na mmoja alishaachika tunaye hapa. Sina chakula wala nguo kama mnavyoniona hata jana hatukula”. Wana THISDASO wamepanga kumtembelea na kutoa huduma nyumbani kwa mzee huyu.
Waweza kutembelea pia    thisdasouniversityofarusha.blogspot.com

waliojitoa wakiwa katika darasa la kuchunguza maandiko chini ya Katibu wa THISDASO ndugu Mwizuka Tilunganyila.

No comments:

Post a Comment