Friday, February 10, 2012


BAADA YA WASABATO KUVAMIA MASHAMBA SASA WAVAMIA SHULE NA KUPORA.

                      Na Juma Kibona-Mwandishi.
                       Baada ya wale wainjilisti wasabato kukutwa wakivamia mashamba na kufanya kazi ya kusaidia kazi za kuvuna (kama wanavyoonekana pichani) sasa wameongezea mtindo mwingine na kupora akili za wanafunzi wote wa kuanzia kidato cha kwa nza hadi cha nne.
                      Hilo limejitokeza katika shule ya sekondari ya Momela baada ya wana THISDASO kuamua kujitolea kufundisha kila siku za kazi asubuhi hadi mchana kabla ya kuanza mikutano ya jioni ya kila siku. mbinu hiyo imeonesha mafanikio makubwa kwani wanafunzi hao wamejikuta wakihudhuria karibu wote na huku wakitoka bila kusahau kujaza kadi za ubatizo.
                      Bila kujielewa walimu wa shule hiyo wameacha vipindi vyote kwa walimu hawa wasabato. wanafunzi wengi wamegundulika kujaza na kwa dhati kusubiri ubatizo.Athari zilizoipata shule hiyo ni pamoja na ratiba ya shule kupangwa upya kwa kufuata vile wasabato hao wapendavyo. hata hivyo vipindi vyote kwa sasa huanza na maombi kabla ya kuendelea na somo.
                      Wakati huo huo imeonekana kuwa wanachama zaidi wanahitaji vipindi. vijizuu kadhaa hugawiwa kwa wanafunzi kila siku. Head Master wa muda (Salimu Nyisarya) amekaririwa akisema, "Shule hii tutaihubiri na kufundisha hadi kieleweke".

No comments:

Post a Comment