Friday, June 15, 2012
WAVULANA MAARUFU NA
WAZURI.
By Mwalimu KIBONA.
Kwanza kabisa asante kwa moyo wako wa
kushirikiana nami na kuruhusu majibu yako niyaweke katika blog japo kwa
ufupisho tu. Pili nakushauru tu kwamba si wewe wa kwanza kuwa maarufu na hata
hivyo mimi sioni kama wewe ni maarufu. Kwa lipi una umaarufu ? Nichokitathmini
kwa haraka wewe ni mzuri na unao mvuto kwa mabinti. Unavyokausha kana kwamba
bado upo upo unawaumiza wengi na sio vizuri.
Hebu zingatia mambo saba (7)
yafuatayo yatakusaidia zaidi ya mno iwapo utayatafakari.
1. Wewe sio mvulana wa kwanza kuwa
maarufu (japo si maaurufu). Alikuwepo akina Eliya, Hanani, na wengineo
waliokuwa maarufu katika ujana wao na waliishi Yerusalemu (I Nyakati 8:28), Androniko
na Yunia walikuwa vijana maarufu kipindi cha agano jipya (Warumi 16:7).
2. Walikuwepo Wavulana wazuri kama Sauli
(I Samweli 9:2), Daudi ( I Samweli 16:18), Musa (Matendo 7:20), na wengineo
wengi.
3. Unaposoma habari za ndoa za hao wote
(wavulana Maarufu na Wazuri hapo juu) wengi wao ndoa zao ziliwasumbua sana, hazikuwa
vile Wavulana wengi maarufu kama wewe wanavyotarajia.
4. Wavulana wote maarufu hupenda kuoa
wanawake ambao dunia itasema hakika amepata kitu chenyewe kama yeye mwenyewe
alivyo wa juu.
5. Ili kuunoesha ulimwengu kuwa wameoa
wavulana maaurufu hupenda kuoa wasichana walio kama wao kwa elimu, kipato,
umaarufu n.k jambo ambalo ni kosa kubwa.
6. Biblia imesema mke amtii mume (soma Waefeso
5:22-24) Kutiiwa ndio sumu kali inayowavuta wanaume kwa wanawake wa nje ni
jambo ambalo likifanywa na mke wa ndani ndoa huwa bora na yenye kunenepesha
moyo. Mke anapaswa kumfanya mme kama moja ya watoto wake jambo ambalo haliwezi
kutendwa na msichana mnayelingana naye elimu, umri, urefu, kipato n.k. (kivipi – tuwasiliane kwa e mail)
7. USHAURI – Uzoefu unaonesha kuwa
ukitaka kupata mke ambaye atakuwa mke, unatakiwa kutafuta msichana unayemzidi
kwa kila kitu yaani kipato, umri, urefu, unene, nguvu, elimu n.k. kwani hayo
yatamjengea hisia za kukutii (rejea namba 6 hapo juu) atakuona uko juu yake
nawe utapata nafasi ya kuonwa hivyo. Pamoja na ukweli huo ni lazima awe mzuri
kwako (anakuvutia). Kwa mfano kama wewe una shahada utatakiwa kuoa mwenye cheti
au stashahada.
NB: Tuwasiliane kwa e mail tupange appointment
kwa ufafanuzi wa hoja saba hapo juu, maana sio rahisi kuanika kila kitu kwenye blog.
Wednesday, June 13, 2012
from .....................
to kibonaticha@yahoo.co.uk
SWALI KWAKO KAKA:
Jina linahifadhiwa kwa ombi la mhusika. Kwanza natoa shukrani kwa kuanzisha huduma hii. Mimi ni kijana wa kiume na kaumri
naona kameenda ila pia kama unavyonifahamu japo kwa umbali nina ka umaarufu
kiasi chake mbona vya kuoa vinanichanganya na ninatamani ila nahisi nitachelewa
sana.
MAJIBU juni
15 TEMBELEA kwaticha.blogspot.com UTAYAKUTA RAFIKI.
Saturday, June 9, 2012
Thursday, June 7, 2012
CHONDE JAMANI TUSIKOMOANE!!!
Na mwandishi wa kujitegemea Kibona.
“Chonde jamani narudia tena chonde” haya ndiyo yalisika toka mdomoni mwa dada mmoja (jina linahifadhiwa). Dada huyo aliendelea kulalamika. “Mtihani gani huu mtu anatunga kitini kizima, halafu anasimamia mno, ina maana tulitakiwa kukariri chote ? aims, strategies na skills looh”.
![]() |
WAKATI WENGINE WAMESIMAMIWA VILIVYO (PICHANI) |
![]() |
WENGINE WAMEENDELEA KUNYWA HUKO NA HUKO (PICHANI) |
Hiyo ndiyo hali iliyotawala mara baada ya mtihani wa kwanza wa HIV. Wanafunzi wengi wameonekana kushtushwa na swali la 31 na 32 hasa baada ya kuona mwelekeo wa kutakiwa kunadika kila kilichomo katika notes. Wengi waliolalamika walikuwa wanafunzi vijana huku wanafunzi watu wazima wakilalamika chinichini. Mwalimu mwanafunzi mama mmoja akasema, “Wazee tutaweza kukariri kweli au ndio kuikosa digrii?”.
Kwa hakika mtihani ulisimamiwa zaidi na wengine kujikuta wakikamatwa wakikopia na kukatwa alama.
Tuesday, June 5, 2012
MITIHANI HIYO IMEFIKA
Jamani mitihani imefika na kila kozi inaonekana kuwa na mchakato mkali hasa mwelekeo wa kusap (supplementary) ambao unaonekana wazi na unamkaribisha kila mmoja. La muhimu ni kwamba tumtegemee yeye anayewezesha tutapita tu.
Hata hivyo hatusahau kuwaombea waliopata ajali huko Mbeya. Waliokufa Muumba anajua lakini walio mahututi bila shaka Bwana atafanya kitu kwa ajili yao.
Nawatakia Maisha mema hapa UoA.
Mwandishi wenu wa kujitegemea.Na KIBONA. Juni 2012
Subscribe to:
Posts (Atom)