WAVULANA MAARUFU NA
WAZURI.
By Mwalimu KIBONA.
Kwanza kabisa asante kwa moyo wako wa
kushirikiana nami na kuruhusu majibu yako niyaweke katika blog japo kwa
ufupisho tu. Pili nakushauru tu kwamba si wewe wa kwanza kuwa maarufu na hata
hivyo mimi sioni kama wewe ni maarufu. Kwa lipi una umaarufu ? Nichokitathmini
kwa haraka wewe ni mzuri na unao mvuto kwa mabinti. Unavyokausha kana kwamba
bado upo upo unawaumiza wengi na sio vizuri.
Hebu zingatia mambo saba (7)
yafuatayo yatakusaidia zaidi ya mno iwapo utayatafakari.
1. Wewe sio mvulana wa kwanza kuwa
maarufu (japo si maaurufu). Alikuwepo akina Eliya, Hanani, na wengineo
waliokuwa maarufu katika ujana wao na waliishi Yerusalemu (I Nyakati 8:28), Androniko
na Yunia walikuwa vijana maarufu kipindi cha agano jipya (Warumi 16:7).
2. Walikuwepo Wavulana wazuri kama Sauli
(I Samweli 9:2), Daudi ( I Samweli 16:18), Musa (Matendo 7:20), na wengineo
wengi.
3. Unaposoma habari za ndoa za hao wote
(wavulana Maarufu na Wazuri hapo juu) wengi wao ndoa zao ziliwasumbua sana, hazikuwa
vile Wavulana wengi maarufu kama wewe wanavyotarajia.
4. Wavulana wote maarufu hupenda kuoa
wanawake ambao dunia itasema hakika amepata kitu chenyewe kama yeye mwenyewe
alivyo wa juu.
5. Ili kuunoesha ulimwengu kuwa wameoa
wavulana maaurufu hupenda kuoa wasichana walio kama wao kwa elimu, kipato,
umaarufu n.k jambo ambalo ni kosa kubwa.
6. Biblia imesema mke amtii mume (soma Waefeso
5:22-24) Kutiiwa ndio sumu kali inayowavuta wanaume kwa wanawake wa nje ni
jambo ambalo likifanywa na mke wa ndani ndoa huwa bora na yenye kunenepesha
moyo. Mke anapaswa kumfanya mme kama moja ya watoto wake jambo ambalo haliwezi
kutendwa na msichana mnayelingana naye elimu, umri, urefu, kipato n.k. (kivipi – tuwasiliane kwa e mail)
7. USHAURI – Uzoefu unaonesha kuwa
ukitaka kupata mke ambaye atakuwa mke, unatakiwa kutafuta msichana unayemzidi
kwa kila kitu yaani kipato, umri, urefu, unene, nguvu, elimu n.k. kwani hayo
yatamjengea hisia za kukutii (rejea namba 6 hapo juu) atakuona uko juu yake
nawe utapata nafasi ya kuonwa hivyo. Pamoja na ukweli huo ni lazima awe mzuri
kwako (anakuvutia). Kwa mfano kama wewe una shahada utatakiwa kuoa mwenye cheti
au stashahada.
NB: Tuwasiliane kwa e mail tupange appointment
kwa ufafanuzi wa hoja saba hapo juu, maana sio rahisi kuanika kila kitu kwenye blog.
No comments:
Post a Comment