CHONDE JAMANI TUSIKOMOANE!!!
Na mwandishi wa kujitegemea Kibona.
“Chonde jamani narudia tena chonde” haya ndiyo yalisika toka mdomoni mwa dada mmoja (jina linahifadhiwa). Dada huyo aliendelea kulalamika. “Mtihani gani huu mtu anatunga kitini kizima, halafu anasimamia mno, ina maana tulitakiwa kukariri chote ? aims, strategies na skills looh”.
![]() |
WAKATI WENGINE WAMESIMAMIWA VILIVYO (PICHANI) |
![]() |
WENGINE WAMEENDELEA KUNYWA HUKO NA HUKO (PICHANI) |
Hiyo ndiyo hali iliyotawala mara baada ya mtihani wa kwanza wa HIV. Wanafunzi wengi wameonekana kushtushwa na swali la 31 na 32 hasa baada ya kuona mwelekeo wa kutakiwa kunadika kila kilichomo katika notes. Wengi waliolalamika walikuwa wanafunzi vijana huku wanafunzi watu wazima wakilalamika chinichini. Mwalimu mwanafunzi mama mmoja akasema, “Wazee tutaweza kukariri kweli au ndio kuikosa digrii?”.
Kwa hakika mtihani ulisimamiwa zaidi na wengine kujikuta wakikamatwa wakikopia na kukatwa alama.
No comments:
Post a Comment