Sunday, June 17, 2012

Friday, June 15, 2012


WAVULANA MAARUFU NA WAZURI.
By Mwalimu KIBONA.
Kwanza kabisa asante kwa moyo wako wa kushirikiana nami na kuruhusu majibu yako niyaweke katika blog japo kwa ufupisho tu. Pili nakushauru tu kwamba si wewe wa kwanza kuwa maarufu na hata hivyo mimi sioni kama wewe ni maarufu. Kwa lipi una umaarufu ? Nichokitathmini kwa haraka wewe ni mzuri na unao mvuto kwa mabinti. Unavyokausha kana kwamba bado upo upo unawaumiza wengi na sio vizuri.
Hebu zingatia mambo saba (7) yafuatayo yatakusaidia zaidi ya mno iwapo utayatafakari.
1.     Wewe sio mvulana wa kwanza kuwa maarufu (japo si maaurufu). Alikuwepo akina Eliya, Hanani, na wengineo waliokuwa maarufu katika ujana wao na waliishi Yerusalemu (I Nyakati 8:28), Androniko na Yunia walikuwa vijana maarufu kipindi cha agano jipya (Warumi 16:7).
2.     Walikuwepo Wavulana wazuri kama Sauli (I Samweli 9:2), Daudi ( I Samweli 16:18), Musa (Matendo 7:20), na wengineo wengi.
3.     Unaposoma habari za ndoa za hao wote (wavulana Maarufu na Wazuri hapo juu) wengi wao ndoa zao ziliwasumbua sana, hazikuwa vile Wavulana wengi maarufu kama wewe wanavyotarajia.
4.     Wavulana wote maarufu hupenda kuoa wanawake ambao dunia itasema hakika amepata kitu chenyewe kama yeye mwenyewe alivyo wa juu.
5.     Ili kuunoesha ulimwengu kuwa wameoa wavulana maaurufu hupenda kuoa wasichana walio kama wao kwa elimu, kipato, umaarufu n.k jambo ambalo ni kosa kubwa.
6.     Biblia imesema mke amtii mume (soma Waefeso 5:22-24) Kutiiwa ndio sumu kali inayowavuta wanaume kwa wanawake wa nje ni jambo ambalo likifanywa na mke wa ndani ndoa huwa bora na yenye kunenepesha moyo. Mke anapaswa kumfanya mme kama moja ya watoto wake jambo ambalo haliwezi kutendwa na msichana mnayelingana naye elimu, umri, urefu, kipato n.k. (kivipi – tuwasiliane kwa e mail)
7.     USHAURI – Uzoefu unaonesha kuwa ukitaka kupata mke ambaye atakuwa mke, unatakiwa kutafuta msichana unayemzidi kwa kila kitu yaani kipato, umri, urefu, unene, nguvu, elimu n.k. kwani hayo yatamjengea hisia za kukutii (rejea namba 6 hapo juu) atakuona uko juu yake nawe utapata nafasi ya kuonwa hivyo. Pamoja na ukweli huo ni lazima awe mzuri kwako (anakuvutia). Kwa mfano kama wewe una shahada utatakiwa kuoa mwenye cheti au stashahada.
NB: Tuwasiliane kwa e mail tupange appointment kwa ufafanuzi wa hoja saba hapo juu, maana sio rahisi kuanika kila kitu kwenye blog.

Wednesday, June 13, 2012


from .....................
to kibonaticha@yahoo.co.uk
SWALI KWAKO KAKA:
Jina linahifadhiwa kwa ombi la mhusika. Kwanza natoa shukrani kwa kuanzisha huduma hii. Mimi ni kijana wa kiume na kaumri naona kameenda ila pia kama unavyonifahamu japo kwa umbali nina ka umaarufu kiasi chake mbona vya kuoa vinanichanganya na ninatamani ila nahisi nitachelewa sana.
MAJIBU juni 15 TEMBELEA kwaticha.blogspot.com UTAYAKUTA RAFIKI.

Saturday, June 9, 2012

UNA SWALI KUHUSU UJANA, MAISHA, NDOA, ELIMU, INJILI, UCHUMI TUMA KWENDA kibonaticha@yahoo.co.uk UTAPOKEA MAJIBU YENYE KUBADILISHA MAISHA.

Thursday, June 7, 2012


MTIHANI ULISIMAMIWA HASA!!!!!! MH KITINI CHOTE.widgets
CHONDE JAMANI TUSIKOMOANE!!! 
                        Na mwandishi wa kujitegemea Kibona. “Chonde jamani narudia tena chonde” haya ndiyo yalisika toka mdomoni mwa dada mmoja (jina linahifadhiwa). Dada huyo aliendelea kulalamika. “Mtihani gani huu mtu anatunga kitini kizima, halafu anasimamia mno, ina maana tulitakiwa kukariri chote ? aims, strategies na skills looh”. 
WAKATI WENGINE WAMESIMAMIWA VILIVYO (PICHANI)
WENGINE WAMEENDELEA KUNYWA HUKO NA HUKO (PICHANI)
                        Hiyo ndiyo hali iliyotawala mara baada ya mtihani wa kwanza wa HIV. Wanafunzi wengi wameonekana kushtushwa na swali la 31 na 32 hasa baada ya kuona mwelekeo wa kutakiwa kunadika kila kilichomo katika notes. Wengi waliolalamika walikuwa wanafunzi vijana huku wanafunzi watu wazima wakilalamika chinichini. Mwalimu mwanafunzi mama mmoja akasema, “Wazee tutaweza kukariri kweli au ndio kuikosa digrii?”. Kwa hakika mtihani ulisimamiwa zaidi na wengine kujikuta wakikamatwa wakikopia na kukatwa alama.

MITIHANI IMEPAMBA MOTO, TWAFWAAA


MTIHANI ULISIMAMIWA HASA!!!!!! MH KITINI CHOTE.widgets

Tuesday, June 5, 2012

JAMANI HII MITIHANI TUTAPONA? (KIBONA)
MITIHANI HIYO IMEFIKA
              Jamani mitihani imefika na kila kozi inaonekana kuwa na mchakato mkali hasa mwelekeo wa kusap (supplementary) ambao unaonekana wazi na unamkaribisha kila mmoja. La muhimu ni kwamba tumtegemee yeye anayewezesha tutapita tu. Hata hivyo hatusahau kuwaombea waliopata ajali huko Mbeya. Waliokufa Muumba anajua lakini walio mahututi bila shaka Bwana atafanya kitu kwa ajili yao. Nawatakia Maisha mema hapa UoA. Mwandishi wenu wa kujitegemea.
Na KIBONA. Juni 2012

Sunday, April 1, 2012

Friday, February 10, 2012

BAADA YA KUVAMIA MASHAMBA SASA WASABATO WAVAMIA SHULE NA KUITEKA YOTE.

                Wanachama wa THISDASO wanaendesha efoti kubwa katika kijiji cha Ngarenanyuki. Mkutano huo unahudumiwa na Ndugu Jerard Nyaonge (mahubiri) Juma Kibona (Kaya na familia pamoja na Usiku Projecta) na Mchungaji Mahemebea (Afya) ilianza February 5/2012 na unatarajiwa kuisha tarehe 18/2/2012.
             Mbinu kadhaa zimeibuliwa kama njia ya kufanikisha mkutano huo ni pamoja na kushiriki kuvuna mashamba ya nyanya na mahidni kwa wanakijiji wa Kijiji cha Ngarenanyuki.
          Njia nyingine ni kufundisha katika shule ya sekondari ya Momela ambapo walimu bila kujijua wamejikuta wakiwaachia vipindi vyote wana THISDASO ambao wamepanga ratiba upya na kutawala shule yote huku wakimchagua Headmaster wa muda (Salim Nyisarya).
            Moja ya mkakati ni kuwataka wanafunzi wote kuhudhuria vipindi vya efoti kama sehemu ya masomo yao. Kwa mkakati huo baadhi ya wanafunzi wamejikuta wakiomba kubatizwa.
kusaidia wenye shida, kujitolea kufundisha, kuvuna mashamba ya wanakijiji hizi ni mbinu ambazo zimefaulu sana.
habari hizi zinapatikana pia    thisdasouniversiotyofarusha.blogspot.com
wawakilishi wa chama cha THISDASO wakiwa wametoka kumpa babu na bibi
zawadi za nguo na vyakula tele tele kutokana na michango ya wanachama.



BAADA YA WASABATO KUVAMIA MASHAMBA SASA WAVAMIA SHULE NA KUPORA.

                      Na Juma Kibona-Mwandishi.
                       Baada ya wale wainjilisti wasabato kukutwa wakivamia mashamba na kufanya kazi ya kusaidia kazi za kuvuna (kama wanavyoonekana pichani) sasa wameongezea mtindo mwingine na kupora akili za wanafunzi wote wa kuanzia kidato cha kwa nza hadi cha nne.
                      Hilo limejitokeza katika shule ya sekondari ya Momela baada ya wana THISDASO kuamua kujitolea kufundisha kila siku za kazi asubuhi hadi mchana kabla ya kuanza mikutano ya jioni ya kila siku. mbinu hiyo imeonesha mafanikio makubwa kwani wanafunzi hao wamejikuta wakihudhuria karibu wote na huku wakitoka bila kusahau kujaza kadi za ubatizo.
                      Bila kujielewa walimu wa shule hiyo wameacha vipindi vyote kwa walimu hawa wasabato. wanafunzi wengi wamegundulika kujaza na kwa dhati kusubiri ubatizo.Athari zilizoipata shule hiyo ni pamoja na ratiba ya shule kupangwa upya kwa kufuata vile wasabato hao wapendavyo. hata hivyo vipindi vyote kwa sasa huanza na maombi kabla ya kuendelea na somo.
                      Wakati huo huo imeonekana kuwa wanachama zaidi wanahitaji vipindi. vijizuu kadhaa hugawiwa kwa wanafunzi kila siku. Head Master wa muda (Salimu Nyisarya) amekaririwa akisema, "Shule hii tutaihubiri na kufundisha hadi kieleweke".

Monday, February 6, 2012

MKUTANO WAPAMBA MOTO


WATU 86 WAUNGUA KWA MOTO NGARENANYUKI NA 7 KUFA.

Na Juma Kibona – Mawasiliano THISDASO UOA.
Katika mkutano wa efoti uliofanyika jana 6/2/2012 hapa Ngarenanyuki-USA River – Arusha, watu 86 (watu wazima wageni tu) walihudhuria na hakika walichomwa na neno la Mungu linaloweza kuchoma kila moyo wa mwanadamu. Ilipofika mwisho wa mkutano watu 7 waliamua kuifia dhambi na kufufuka katika utukufu wa Bwana. Aidha wanakijiji hawa, wamekiri kuwa Yesu anawapenda sana. Frolida anasema, “Nimekuwa nikisumbuka sana ili nipate mme nimekuja kuombewa ili niolewe”. Watu wa Mungu waliomba naye na akafurahi kwamba bila shaka Bwana atafanya muujiza.
Efoti hii inaendesha na kusimamiwa na wanachama wa THISDASO tawi la University of Arusha. Mkutano huu ulianza tarehe 5/2/2012 na utamalizikia tarehe 18/2/2012. Mkutano huu umeambatana na matembezi. Ambapo kila siku asubuhi wanachama hawa hutembelea wanakijiji wote wa Ngarenanyuki.
Leo 7/2/2012, kati ya waliotembelewa na Mzee “Selewani” Silvano ambaye ana miaka 130 kama alivyosema. Mzee huyu anasema, “Nilikuwa na watoto 6, wanne kati yao walikuwa wa kiume na walikwishafariki wote kwa tatizo la UKIMWI, wamebaki 2 wa kike ambapo mmoja hajulikani alipo na mmoja alishaachika tunaye hapa. Sina chakula wala nguo kama mnavyoniona hata jana hatukula”. Wana THISDASO wamepanga kumtembelea na kutoa huduma nyumbani kwa mzee huyu.
Waweza kutembelea pia    thisdasouniversityofarusha.blogspot.com

waliojitoa wakiwa katika darasa la kuchunguza maandiko chini ya Katibu wa THISDASO ndugu Mwizuka Tilunganyila.

Thursday, February 2, 2012

NAWASALIMU KATIKA JINA LA BWANA.
                  Taarifa za hivi karibuni zinasema kuwa asubuhi ya Ijumaa ya tarehe 3/2/2012 vijana wa THISDASO wameondoka kwenda Ngarenanyuki kwenye efoti wakati wengine wakiwa wanaelekea Makwao. Akihojiwa mmoja wa wanachama hao aitwaye Leah Karangi amesema "ni kutokana na kuendea mahitaji kwa wazazi inatulazimu kwenda makwetu" Hata hivyo mjumbe wa programu zote Aunt Masegenya au Mama Mkingira naye alikaririwa akisema "Ninawatakia wanachama wote effort njema" Huku akionesha kutamani kuhudhuria.
                              Vijana wa Kisabato wapatao 85 wanahudhuria mkutano huo, aidha mafundisho ya Neno la Mungu yataongozwa na Mwalimu Nnyaonge, Semina za Afya zitaongozwa na Mchungaji na Mwasitete na Semina za Kaya na Familia zitaongozwa na Mwalimu Kibona kutoka Mpanda. Unatarajiwa kuwa mkutano wenye mafanikio.

Find more music like this on G5 world

Find more music like this on G5 world

habari zote za maisha tukutane kwaticha.blogspot.com